Wakenya wahimizwa kuliombea taifa wikendi hii

0

Baraza la kidini linawahimiza wakenya kujiunga kwenye maombi ya kitaifa ya siku tatu ambayo yatakamilika siku ya Jumapili.

Katika taarifa, mwenyekiti wa baraza hilo kasisi Anthony Muheria amewataka wakenya kuliombea taifa kutoka kwa makanisa yao wakizingatia sheria za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Kasisi Muheria pia anawataka wakenya kuombea uponyaji wa kitaifa haswa kutokana na janga la corona na pia kuwaombea viongozi.

Wikendi hii, rais Uhuru Kenyatta ataongoza hafla ya maombi katika ikulu ya Rais Nairobi, hafla ambayo itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa.

Yakijiri hayo

Serikali imetangaza Jumamosi kuwa siku kuu na ambayo itaadhimishwa kupitia maombi ya kitaifa na huduma kwa jamii.

Kwenye taarifa waziri wa usalama Dkt. Fred Matiang’i ametangaza rasmi October 10 kuwa huduma dei.

Matiang’i amesema siku hiyo inastahili kuadhimishwa kupitia maombi ya kitaifa kuonyesha huduma na kujitolea kutoa huduma kwa jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here