Baadhi ya wakaazi wa jiji kuu la Nairobi hawatakuwa na maji kuanzia saa kumi mbili asubuhi hapo kesho hadi siku ya ijumaa.
Kampuni ya maji na maji taka Nairobi imesema ukosefu wa maji unafuatia ukarabati utakaofanyika katika kituo cha kutibu maji cha Ngethu eneo la Mwangu kando ya mto Chania.
Miongoni mwa maeneo yatakayoathirika ni katikati mwa mji mkuu ,chuo kikuu cha UON, JKIA ,Mombasa ,Juja, Jogoo, Outering na mitaa iliyoko barabara za Kangundo na Thika.
Miongoni mwa mitaa hiyo ni eneo la viwnadani, Mlango Kubwa, Mathare, Eastleigh, Moi Airbase, Huruma, Kariobangi, Pangani, Maringo, Buruburu, Bahati, Outer-Ring, Baba Dogo, Dandora, Umoja, Donholm, Fedha, Ngong, Naivasha na Kikuyu.