Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu amekosa kufika mahakamani kwa vikao vya kuskilizwa kwa kesi ya ulaghai inayomkabili.
Kupitia kwa Wakili wake, Waititu ameiambia mahakama kuwa amepatwa na virusi vya corona na hivyo hawezi kufika mahakamani.
Waititu ambaye alitimuliwa na waakilishi wadi anasema kwa sasa amejitenga akiendelea kupokea matibabu ya virusi hivyo.