Wahudumu wa afya 945 wameambukizwa corona

0

Watu wengine 183 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi visa hivyo nchini kuwa 36,576.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amesema idadi hiyo ni kutokana na sampuli 4, 188 zilizopimwa.

Aidha, wagonjwa watano zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 642 huku idadi ya waliopona ikifikia 23,611.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 54, Kisumu 26, Trans Nzoia 16, Mombasa 20, Kericho 11, Nakuru 10, Machakos 6, Kajiado, Busia 2, Kakamega na Embu 1.

Hayo yakijiri

Takriban wahudumu wa afya 945 wameambukizwa virusi vya corona tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa nchini mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi anasema wahudumu wa afya wapatao 16 wamefariki kutokana na ugonjwa nchini huku siku ya  kuangazia usalama wao ikiadhimishwa leo.

Na huku wahudumu wa afya wakilalamikia ukosefu wa vifaa vya kujikinga wanapowashughulikia wagonjwa wa COVID19, Dkt. Mwangangi amesema serikali imejitahidi kuhakikisha kuwa wanapata vifaa hivyo ili kuwawezesha kujikinga.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here