Wahudumu wa afya Homabay wasitisha mgomo

0

Wahudumu wa afya katika kaunti ya Homa Bay wanatazamiwa kurejea kazini baada ya kusitisha mgomo wao uliodumu kwa muda wa mwezi mmoja.

Hii ni baada yao kuafikia makubaliano na serikali ya kaunti hiyo kuhusu mishahara na marupurupu ya mwezi Juni na Julai.

Nao madaktari katika kaunti ya Kericho wametoa makataa ya siku 14 kugoma baada ya serikali ya kaunti hiyo kukosa kutekeleza mkataba wa maelewano baina yao.

Kupitia kwa muungano wa madaktari KMPDU tawi la Kericho, wahudumu hao wa afya wanasema serikali ya Kericho imekataa kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuongezwa mishahara na kutowapandishwa vyeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here