Wahudumu wa afya 1,029 waambukizwa corona Kenya, 16 wafariki

0

Wahudumu wa afya wapatao 1,029 wameambukizwa virusi vya corona tangu kisa cha kwanza kiripotiwe nchini mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Haya yamesemwa na katibu wa wizara ya afya Dkt Rashid Aman amesema kati yao ni wanaume 526 na wanawake 503.

Idadi ya madaktari na wauguzi waliofariki kutokana na ugonjwa huo inasalia kuwa 16.

Kwa kuzingatia maambukizi ya ugonjwa huo katika kaunti, Nairobi inaongoza na 20,971, Mombasa ni ya pili kwa visa 2,969 ikifuatiwa na Kiambu iliyorekodi visa 2,776, Kajiado ni ya nne na visa 1,981, Machakos ni ya tano na 1,340, kaunti ya Nakuru ni ya sita kwa kuandikisha visa 1,259  huku Busia ikiwa ya saba kwa kuandikisha visa 1,246.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here