Takribani wahamiaji elfu mbili walio humu nchini wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo kudhulumiwa, haki zao msingi kukiukwa haswa wakati wanatiwa nguvuni na maafisa wa usalama na pia kubaguliwa wakiwa gerezani.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibindamanu KNCHR ambapo wahamiaji 246 na maafisa wa polisi 175 walihojiwa.
Ripoti iliyotolewa na shirika hiyo inaonesha kuwa wahamiaji wanazuiliwa katika maeneo yaliyo katika hali mbaya huku uhuru wao ukiminywa wanapokamatwa.
Akizunguzma wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurungezi mkuu wa tume hiyo Veronica Mwangi amesema maafisa wa polisi waliojukumika kuwalinda wahamiaji hao wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kutoelewa lugha wanazozungumza wahamiaji hao na ukosefu wa mafunzo maalum.
Kwa mujibu wa tume hiyo, serikali hutumia takribani shilingi billion mbili kila mwaka kuwashughulikia wahamiaji ikiwemo kuwarudsiha makwao kwa lazima.
Asilimia 65% ya wahamiaji hao ni raia wa Tanzania, Uganda, Somalia na Ethiopia kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, wahamiaji wanaopatikana nchini kinyume cha sheria wanafaa kutozwa faini isiyozidi shilingi nusu million au wahudumie kifungo cha hadi miaka mitatu.
Mwangi anasema watatumia utafiti huu kuishawishi serikali na washikadau wengine kufanya marekebisho yanayofaa katika sekta hiyo ili kulinda haki za wahamiaji.