Wagonjwa 14 zaidi wafariki kutokana na corona

0

Wagonjwa 14 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa Corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita  na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,545.

Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amethibitisha kuwa Idadi ya waliopona imeongezeka na kufika 69,839 baada ya watu 425 kupona kutokana na virusi hivyo.

Watu 521 wameambukizwa virusi hivyo baada ya sampuli 4,721 kupimwa na hivyo kufikisha idadi ya maambukizi kuwa 89,100.

Wagonjwa 1,102 wamelazwa katika hospitali mbalimbali wengine 8,016 wakiwa kwa matibabu ya nyumbani.

Watu 71 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi na 31 wanasaidiwa na mashine kupumua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here