Wafanyikazi wa duka la jumla la Tuskys wameandanana jijini Nairobi na mjini Eldoret kulalamikia kutolipwa mishahara yao kuanzia mwezi Julai mwaka huu.
Jijini Nairobi wafanyikazi hao wameandamana katika barabara mbalimbali katikati mwa jiji na kudai kuwa badala ya kulipwa pesa zao, usimamizi wa duka hilo umewapa barua za kuonyesha kuwa wamefutwa kazi.
Mjini Eldoret, wafanyikazi hao wanasema wako tayari kufutwa kazi mradi walipwe pesa zao za miezi mitatu walizofanyia kazi.
Inaripotiwa kuwa duka hilo la Tuskys lina madeni mengi ikiwemo ya wasambazajI bidhaa na kodi za wamiliki wa majengo yaliyo na biashara zao.