Wafanyikazi 41 Pumwani wapatikana na corona

0

Maafisa kutoka wizara ya afya wamezuru hospitali ya akina mama kujifungulia ya Pumwani kutathmini hali baada ya wafanyikazi 41 ikiwemo wahudumu wa afya kupatikana na virusi vya corona.

Mkurugenzi wa matibabu Patrick Amoth anasema wafanyikazi hao wanaendelea vema na matibabu na tayari wawili wamepona na kuruhusiwa kuenda nyumbani.

Kwa mujibu wa Amoth, jumla ya wahudumu wa afya 429 wamemabukizwa virusi vya corona nchini, hii ikiwa ni asilimia 4.1% ya maambukizi yote ya corona nchini.

Amoth ametoa hakikisho kwa umma kuwa wamewasilisha vifaa vya kutosha vya kujilinda kwa wahudumu wa afya wanapokuwa kazini katika hospitali hiyo ya Pumwani na kuwahakikishia wamama wajawazito kuwa watapata huduma bora.

Ijumaa wiki iliyopita, Dr Doreen Adisa Lugaliki alikuwa Daktari wa kwanza kufariki baada ya kuambukizwa corona akiwa kazini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here