Wadau wapinga BAT kuondolewa ushuru

0

Serikali ya Kenya imetakiwa kukataa ombi la kampuni ya kuuza bidhaa za tumbaku kutoka Uingereza BAT kutaka kuruhusiwa kutolipa ushuru kwa muda wa miaka mitatu.

Wadau mbalimbali wanaopinga matumizi ya bidhaa za tumbaku wakiongozwa na KETCA chini ya uongozi wake Joel Gitali wanahoji kuwa hatua hiyo itachangia katika matumizi ya bidhaa za tumbaku na hivyo kuathiri afya ya wengi.
Selin Awuor kutoka shirika la International Institute for Legislative Affairs anatoa maoni sawa na hayo akisema hatua hiyo itatoa nafasi ya kuuzwa kwa bidhaa za tumbaku katika maeneo tofauti nchini na kufanya rahisi kwa bidhaa hizo kupatikana kokote.

Wanahoji kuwa iwapo kampuni hiyo itazuiliwa kulipa ushuru, watakaoathirika zaidi ni watoto kwani bidhaa hizo zitaanza kuuzwa kiholela.

Gitali amezitaka wizara ya afya kuwa katika mstari wa mbele kupinga matumizi ya bidhaa za tumbaku kwa kuzingatia madhara yake kwa afya ya watumizi wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here