“WACHENI SIASA ZA MAPEMA” MALALA AFOKEA MAWAZIRI NA WABUNGE

0
KATIBU MKUU WA UDA CLEOPHAS MALALAA

Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala ameshtumu mawaziri Moses Kuria (Utumishi wa Umma) na Kipchumba Murkomen (Uchukuzi) kwa kujihusisha na siasa.

Malala ametaka wawili hao kujiuzulu kutoka kwa nyadhifa zao akisema nafasi wanazoshikilia zinawahitaji kutojiuhusisha kivyovyote vile na siasa.

“Waziri Kuria jukumu lako kuu ni kuhakikisha huduma ya umaa inafanya kazi ipasavyo. Iwapo unataka kujihusisha na siasa basi jiuzulu” Malala amesema.
Wawili hao hususan waziri Kuria wamekuwa wakitoa kauli zinazoonekana kumkejeli naibu wa Rais Rigathi Gachagua.

Seneta huyo wa zamani wa Kakamega amesema ni sharti viongozi wote wa chama hicho tawala wapewe heshima wanaostahiki.

Hayo yanajiri kwa wakati ambapo kuna mvutano kati ya wandani wa Rais na naibu wake baada ya kuibuka kwa madai ya kutengwa kwa naibu wa Rais serikalini.

Malala aidha ameonya viongozi ‘wachanga’ wanaorindima siasa za uridhi mwaka wa 2032 akisema ni mapema sana kwa mjadala kuhusu uridhi kuangaziwa kwa sasa.
Malala ametaka viongozi hao kuweka ruwaza yao katika kutimiza majukumu kwa mpiga kura aliyewachagua katika uchaguzi mkuu uliopita.

“Iwapo mutaendelea na siasa, chama hakitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu” Ameonya seneta huyo wa zamani wa Kakamega.
Kauli ya Malala inakuja wakati ambapo pana mgawanyiko ndani ya UDA upande mmoja wa chama hicho ukiegemea kwa mrengo wa Rais William Ruto na upande mwingine ukivutia upande wa Naibu wake Rigathi Gachagua.

Mpasuko chamani humo ulijidhihirisha wazi kwa mara ya kwanza baada ya wandani wa Gachagua kudai kuwa anatengwa serikalini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here