Wabunge wataka maelezo kuhusu kukamatwa kwa mwanahabari Yassin Juma

0

Bunge la kitaifa linataka maelezo kamili kuhusu ni kwa nini mwanahabari Yassin Juma alishikwa na kuzuiliwa nchini Ethopia kwa siku 46.

Wabunge hao wakiongozwa na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Taita Taveta Lydia Mizighi wanataka maelezo kamili kutolewa ili Wakenya wafahamu kilichosababisha kukamatwa na kuzuiliwa kwa mwanahabari huyo.

Wabunge hao wanasema mazoea ya Wakenya kuhaingaishwa katika mataifa mengine yanafaa kukoma na kwamba serikali ni sharti ijitahidi kushughulikia maslahi ya raia wake walio nje ya nchi.

Mwanahabari huyo aliachiliwa huru baada ya mazungumzo baina ya mataifa haya mawili kufuatia shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali likiwemo shirika la vyombo vya habari nchini MCK.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here