Wabunge waliostaafu watalipwa pensheni ya kima cha Sh100, 000 kila mwezi baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha mswada wake kiongozi wa walio wachache bungeni John Mbadi.
Wakiidhinisha mswada huo, wabunge hao akiwemo kiranja wa walio wachache Junet Mohamed walihoji kwamba wenzao waliostaafu wanapitia kwenye hali ngumu ya maisha na hata baadhi yao wamekosa hela za matibabu wanapokuwa wagonjwa.
Kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Amos Kimunya vile vile aliunga mkono mswada huo akisema itakuwa sawa kwa wenzao waliostaafu kupata kiinua mgongo baada ya kulihudumia taifa.
Hii ina maana kwamba wabunge 375 wastaafu na waliohudumu kati ya mwaka 1984 na 2001 wataanza kupokea Sh100, 000 iwapo rais atatia kidole kwenye mswada huo.