Wabunge waishambulia Infotrack

0

Utafiti wa hivi punde wa kampuni ya Infotrack uliowataja wabunge wachapa kazi na wale wazembe umeibua tumbo joto bungeni huku wabunge wakipinga matokeo ya utafiti huo.

Wabunge wakiongozwa na Mille Odhiambo wa Suna Kaskazini na Elisha Odhiambo wa Gem wameikemea kampuni hiyo ya Infotrack kutokana na kile wametaja kama kuwaharibia jina kwa kueneza porojo pasipo kuwa na ushahidi kuhusu utendakazi wao.

Baadhi ya wabunge wamedai kuitishwa hongo na kampuni hiyo ili kuorodheshwa miongoni mwa wale wanaofanya vyema kwa kutumia pesa za ustawishaji maeneo bunge CDF.

Utafiti huo ulimuorodhesha mbunge wa Emuhaya Omboko Milemba kileleni kwa asilimia 74% huku Abdi Koroputepo wa Isiolo Kusini akiburura mkia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here