Wabunge, Ndindi Nyoro wa Kiharu na Alice Wahome wa Kandara wametakiwa kufika katika afisi za idara ya upelelezi nchni DCI kurekodi taarifa kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa katika eneo la Kenol kaunti ya Muranga na kusababisha maafa ya watu wawili.
Katika taarifa, DCI inasema wawili hao miongoni mwa washukiwa wnegine wana hadi asubuhi hii kufika katika afisi zake kaunti ya Nyeri kuandikisha taarifa kuhusiana na vurugu hizo.
Wawili hao wanadaiwa kufadhili kundi la wahuni ambao walizua vurugu kabla ya ziara ya naibu Rais Williamn Ruto katika kanisa la AIPCA kuchangisha pesa.
Inspekta muu wa polisi Hillary Mutyambai ametoa wito kwa wanasiasa kukoma kutoa matamshi ya uchochezi na kusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.