Wanaume wanne waliohukumiwa nchini India kwa kumbaka kwa awamu na kumuua mwanafunzi mjini Delhi mwaka 2012 wamenyongwa.
Mahakama iliwahukumu wanne hao Akshay Thakur, Vinay Sharma, Pawan Gupta na Mukesh Singh mnamo mwaka 2013.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 23 alikufa kutokana na majeraha baada ya kubakwa na wanaume sita kwenye basi lililokuwa linaendeshwa.
Kisa hicho kilisababisha maandamano na kuanzishwa kwa sheria za kupambana na ubakaji India.