Polisi mjini Nakuru wametumia vitoa machozi kutawanya maandamano ya wanaharakati wanaolalamikia wizi wa mali ya umma katika shirika la KEMSA.
Waandamanaji hao wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kusimama kidete kulinda mali ya umma na kuhakikisha kuwa wanaopora pesa za mlipa ushuru wanakamatwa na kushtakiwa.
Wanaharakati hao pia wanashtumu serikali ya Gavana Lee Kinyanjui kwa kutumia vibaya pesa zilzotengwa kukabiliana na janga hilo.
Baadhi ya wanaharakati hao wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukiuka masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.
Maandamano sawia na hayo yamefanyika katika kaunti ya Kisumu, ila hapa maafisa wa polisi wamewaruhusu kueleezea lalama zao bila kuwarushia vitoa machozi.
Wiki iliyopita, maandamano sawia na hayoyalifanyika jijini Nairobi na pia kusambaratishwa na polisi kwa kutumia vitoa machozi.