Vurugu zashuhudiwa Migori

0

MCA mmoja wa Migori anauguza majeraha kufuatia kuibuka kwa vurugu katika bunge la kaunti la kaunti hiyo baada ya wawakilishi wadi kutoafikiana kuhusu kurejeshwa kwa mwenzao wa  Kanyamkago Kaskazini George Omamba. 

Omamba ameteuliwa kama naibu spika hii ni baaada ya naibu spika kudaiwa kuwa mgonjwa

Haya yanajiri huku bunge hilo likitazamiwa kujadili hoja ya kumtimua gavana wa kaunti ya Migori Zachary Okoth Obado aliyeshtakiwa kwa ufisadi.

Chama cha ODM kiliidhinisha kuwasilishwa kwa hoja ya kumbandua gavana Obado kufuatia kushtakiwa kwake kuhusiana na ufujaji wa Shilingi Milioni 73 ambapo alizuiliwa kuingia afisini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here