Wizara ya Afya imetangaza kugunduliwa kwa wagonjwa wapya watano wa Mpox na kufikisha jumla ya angalau 28.
Kesi hizo mpya, kulingana na Waziri Deborah Barasa, ziliripotiwa kutoka kaunti ya Nakuru ambapo kesi tatu zilipatikana huku visa viwili vikiripotiwa Mombasa.
Orodha ya kaunti zilizo na visa vya Mpox ni kama ifuatavyo; Nakuru (9). Mombasa (6) Kajiado (2), Bungoma (2), Nairobi (2), Taita Taveta (1), Busia (1), Kiambu (1), Makueni (1), Kericho (1), Uasin Gishu (1) , na Kilifi (1).
Kwa sasa, watu wanane (8) wako chini ya uangalizi , 17 wamepona kabisa, huku wawili (2) wakiwa wamejitenga huku mtu mmoja akiaga kutokana na ugonjwa huo.
“Jumla ya wasafiri 2,207,715 wamepimwa katika Vituo mbalimbali vya Kuingia (POE), tangu kuanza kwa mlipuko huo Julai 2024. Maabara ya Kitaifa ya Afya ya Umma (NPHL) hadi sasa imepokea sampuli 322 za kupimwa, 28 kati yao zimepimwa chanya, 292 wamechapisha matokeo hasi na mawili yanasubiri,” amesema.
Wizara ya Afya imetahadhari umma kuepuka kuwasiliana kwa karibu na watu walio na ugonjwa unaoshukiwa au uliothibitishwa.