Visa vya corona vyaendelea kupungua Kenya

0

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini imeongezeka na kufika 37,079 baada ya watu 98 zaidi kupatikana na virusi hivyo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu mkuu wa wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amedhibitisha kuwa watu 62 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa 23,949.

Idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa huo imefika 650 baada ya watu wawili zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zillizopita.

Nairobi bado inaongoza na visa 32, Mombasa 20, Meru na Uasingishu 8, Kiambu 5, Kisumu na Machakos 4, Kwale, Garissa, Samburu na Nakuru 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here