Visa vipya 492 vya ugonjwa corona vimedhibitishwa baada ya kupima sampuli 4,063 na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 26,928.
Nairobi ingali inaongoza katika msambao wa virusi hivyo kwa kuripoti visa 357, Garissa 52, Kiambu 37, Kajiado 14, Machakos 10, Busia 5,Baringo, Mombasa, Embu na Murang’a 3, Kilifi 2 huku Isiolo, Makueni & Uasin Gishu wakiripoti kisa kimoja kila mmoja
Watu wengine 534 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 13,485 huku watu watatu zaidi wakifariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 424.
Jijini Nairobi, Langata imerekodi visa 76, Embakasi West 28, Makadara 24, Embakasi East 22, Ruaraka 22, Dagoreti North na Roysambu 21, Westlands 19, Embakasi South 17, Kamukunji, Kasarani & Starehe 16, Dagoreti South na Kibra 14, Mathare 11, Embakasi Central na Embakasi North 10,