Idadi ya visa vya ugonjwa wa corona nchini imeongezeka na kufikia 24, 411 baada ya watu wengine 538 kupatikana na virusi hivyo.
Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema visa hivyo vimeongezeka baada ya kupima sampuli 6,195 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Nairobi imerekodi visa 277, Kiambu 72, Kajiado 55, Nakuru 25, Mandera, Laikipia & Bomet 6 kila mmoja.
Watu wengine 514 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 10, 444 huku watu wengine 8 wakifariki na kuongeza idadi ya maafa kuwa 399.
Westlands inaongoza Nairobi kwa kurekodi visa 32, Kasarani 23, Dagoreti North na Ruaraka 21, Embakasi South 19, Roysambu 18 na Kibra 16.