Visa vya corona Kenya vyazidi kupanda

0

Watu 245 wamepatikana na ugonjwa wa corona baada ya kupima sampuli 3,150 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman anasema hii inafikisha 30,365 idadi ya visa vya ugonjwa wa corona kufikia sasa.

Wagonjwa wengine 504 wamepona kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 17,160 huku maafa yakifikia 482 baada ya wagonjwa nane zaidi kufariki.

Nairobi imeandikisha visa 149, Kiambu 23, Kajiado 14, Mombasa 10, Garissa & Machakos 9, Meru & Narok 7, Busia 4, Kilifi 3, Laikipia, Murang’a na Kitui 2, Kisumu, Uasin Gishu, Kwale & Tharaka Nithi 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here