Visa vya corona Kenya vyaendelea kupungua

0

Wizara ya afya imeashiria kwamba taifa la Kenya liko katika mwelekeo unaofaa katika vita dhidi ya ugonjwa wa corona.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema kwa kuzingatia kupungua kwa idadi ya visa vinavyoripotiwa kila siku, taifa liko katika mwelekeo unaofaa kuambatana na mahitaji ya shirika la afya duniani WHO.

Mtoto wa miaka mitatu ni miongoni mwa watu 130 waliopatikana na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 37,348.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema watu 106 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa 24,253.

Aidha, idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa huo imeongezeka na kufikia 664 baada ya watu 5 zaidi kufariki.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 35, Kiambu 23 , Kisumu 19, Mombasa 14, Uasin Gishu 8, Kericho 6, Busia, Kilifi na Kisii 5, Bomet na Narok 2, Turkana, Meru, Machakos, Trans Nzoia, Kajiado na Siaya 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here