Viongozi wakemea tukio ambapo wakili alikufa baada ya kukatwa mikono

0

Viongozi mbali mbali katika kaunti ya Makueni wanaendelea kulaani kisa kilichopelekea kifo cha wakili Onesmus Masaku.     

Wakizungumza katika sherehe za Mashujaa katika kaunti ya Makueni na kuongozwa na kamishna wa kaunti hiyo Mohamed Maalim, viongozi hao akiwemo mbunge wa Makueni Dan Maanzo wametaja kisa hicho kama cha kinyama na kutaka wahusika wakuu kuchukulia hatua za kisheria.

Afisa wa polisi wa kike Nancy Njeri anayedaiwa kumkata mikono wakili huyo tayari amesimamishwa kazi.

Ripoti ya polisi ilidai kuwa Konstabo Njeri alimkata mikono wakili huyo kufuatia jaribio la ubakaji, msimamo ambao ulipingwa baadae na watetezi wa haki za kibinadamu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here