Viongozi wa Jubilee watakiwa kukomesha siasa za matusi

0

Naibu rais William Ruto amewataka watumishi wa umma kukoma kupiga siasa na badala yake walenge kuwahudumia Wakenya ili kutimiza ajenda ya chama tawala cha Jubilee.

Akionekana kurejelea matusi baina ya waziri wa Mazingira Keriako Tobiko na seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, Ruto amesema lililo muhimu kwa sasa ni serikali kutimiza ahadi ilizotoa kwa Wakenya msimu wa kampeini za uchaguzi mkuu.

Naibu rais amesema haya baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la ACK St. Pauls Athi River katika kaunti ya Machakos.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here