‘Vasco’, mshukiwa aliyemdanganya msichana wa shule ashikwa

0

Marcos Menza Masumbuko, jamaa anayehusishwa na kupotea kwa mwanafunzi wa darasa la nane ameshikwa na makachero wa idara ya upelelezi (DCI).

Mshukiwa mwenye umri wa miaka 23 amekamatwa katika kituo cha Polisi cha Mathare ambapo anadaiwa kumdanganywa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.

Uchunguzi wa DCI uliwaelekeza hadi kwenye mtandao wa Facebook ambapo Masumbuko alimtumia mwanafunzi huyo ombi la kuwa rafiki naye kabla ya kumdanganya na kumpeleka katika nyumba yake.

Mshukiwa anayefahamika na wengi kama ‘Vasco’ anadaiwa kuishi na mwanafunzi huyo kwa muda kabla ya kumsaidia kutoroka hadi kwa shangaziye anayeishi Nyakach.

Vasco anasemakana kunyoa nywele zake rasta pindi mtoto huyo alipopotea ili kujifinya asikamatwe.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here