Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga anasema shughuli ya kuanza kukusanya sahihi milioni moja za kubadilisha katiba kupitia mchakato wa BBI itazinduliwa Alhamisi hii.
Odinga anasema uzinduzi huo unatazamiwa kuongozwa na rais Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza safari ya kuelekea kwa kura ya maamuzi mwaka ujao.
Kiongozi huyo wa upinzani amesema haya baada ya kukutana na viongozi wa wengi na wachache katika mabunge yote arobaini na saba.
Baada kukusanywa kwa sahihi hizo, kundi litakaloongoza mchakato huo litazipeleka kwa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kukaguliwa kabla ya kuwasilisha mswada huyo kwa mabunge ya kaunti kupigiwa kura.
Kisheria, mswada huo unapaswa kuungwa mkono angalau na mabunge ya kaunti yapatayo Ishirini na nne chini ya muda wa miezi mitatu.