Gavana wa Kakamega Wycliffe Ambetsa Oparanya ameorodheshwa kuwa wa kwanza katika utendakazi ikilinganishwa na magavana wengine 46.
Katika utafiti huo uliotolewa na shirika la Infotrak, Oparanya ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana amepata asilimia 82.3% akifuatiwa kwa karibu na Gavana wa Kwale Salim Mvurya kwa asilimia 77.1%.
Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana ni wa tatu kwa asilimia 74.4%.
Magavana Alfred Mutua (Machakos),Anyang Nyongo (Kisumu), John Lonyangapuo (Pokot Magharibi), Jackson Mandago (Uasin Gishu), Muthomi Njuki (Tharaka Nithi), Josphat Nanok (Turkana) na Hillary Barchok (Bomet) wanafunga kumi bora kwa utendakazi wao.
Kuhusu maendeleo katika kaunti; Kakamega bado ni kIfua mbele kwa asilimia 57.2%, Kwale 54.8%, Makueni 54.7%, Kisumu 53.4%, Uasin Gishu 53.1%, Pokot Magharibi 52.7% na Elgeiyo Marakwet 51.2%.
Kaunti ya Tana River Dhado Godhana inashika mkia kwa utendakazi ambapo imeorodheshwa ya mwisho kwa kuwa na asilimia 39.5%.