Usihusishe siasa za 2022 na BBI, Rais Kenyatta amuambia Ruto

0

Rais Uhuru Kenyatta amewataka wanasisasa kuepusha siasa za mapema za 2022 na mchakato mzima wa kufanyia katiba marekebisho kupitia ripoti ya maridhiano BBI.

Akimlenga moja kwa moja naibu wake William Ruto, rais Kenyatta amesema muhimu kwa sasa ni kuafikia umoja wa kitaifa kupitia marekebisho hayo na wala sio kulumbana kuhusu uchaguzi mkuu.

Rais Kenyatta ameendelea kupigia debe ripoti hiyo akisema lengo lake ni kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikilikumba taifa hili kwa muda mrefu kila baada ya uchaguzi.

Kauli zake zimeungwa mkono na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ambaye amesema lengo lao sio kupanga namna ya kugawana viti wakati wa uchaguzi mkuu wa 2022 ila ni kuwaleta Wakenya wote pamoja.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here