USHAHIDI DHIDI YA MACKENZI WAWASILISHWA MAHAKAMANI

0

Mahakama ya Shanzu mjini Malindi imefahamishwa jinsi mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie alivyoendesha kundi la liuhalifu lililosababisha maafa ya watu angalau 400 kwenye msitu wa Shakahola huko Kilifi.

Hakimu mkuu wa mahakama hiyo Leah Juma amepata kuskia jinsi kundi hilo kwa kuvalia ngozi ya kanisa lilivyoendesha shughuli zake kupitia itikadi kali.

Upande wa mashtaka umehoji kwamba kundi hilo lilitekeleza mauaji kwa mbinu iliyojumuisha mipango kabambe ya mawasiliano, usafiri na usalama ili kuwalazimishia wafuasi mafunzo ya Mackenzie.

Naibu wa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Jami Yamina amedokeza upande wa mashtaka itakuwa inawasilisha ushahidi ulioko kwenye mfumo wa kielektroniki na kidijitali kando na kuwasilisha mashahidi 90.

Kulingana na Yamina mashahidi wataelezea mahakama kwa kina na kuchora picha ya jinsi mauaji yalitekelezwa kwenye msitu wa Shakahola.

“Katika kuwasilisha ushahidi wa kudhihirisha mashtaka dhidi ya washukiwa, mashahidi wataelezea na kuidhinisha madai yanayoambatana na mashtaka” Yamina ametaja.

“Ushahidi huo utaweka wazi jinsi kwa kuitikia mafunzo ya Mackenzie ilikuwa ni kutia saini cheti cha kifo na kufanyika kuwa shujaa kupitia matendo ambayo yanaorodheshwa kama mauaji au mauaji bila kukusudia” Yamin ameongeza.

Aidha upande wa mashtaka utakuwa unawasilisha ripoti za uhalifu wa kimitandao na maoni ya wataalam ili kudhihirisha vile waadhiriwa walidhulumiwa hata kihisia kutokana na injili lya itikadi kali.

Mahakama imejullishwa Mackenzie na naibu wake Smart Deri Mwakalama ndio washukiwa wakuu wa mauaji ya watoto na wanawake ambao hawakuwa na wakuwatetea.

Upande wa mashtaka imependekezea mahakama kuzuru msitu wa Shakahola ili kupata picha kamili ya eneo la uhalifu huku ukitoa hakikisho la ushahidi dhabiti wa kudhihirisha washukiwa wote 95 walihusika na mauaji hayo.

Mackenzi na washukiwa wenza 94 wanakabiliwa na mashtaka 13 ya ugaidi yanayohusishwa na vifo vya watu Zaidi ya 436 ambao miili yao imefukuliwa kutoka msitu wa Shakahola.

Mahakama ya Shanzu imeratibu mashahidi kutoa ushahidi wao kati ya Jumatatu na Alhamisi huku ushahidi Zaidi ukitarajiwa kusikilizwa kati ya terehe 22 na 25 mwezi Julai mwaka wa 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here