Upinzani Tanzania wapinga ushindi wa Magufuli, waitisha maandamano Jumatatu

0

Upinzani nchini Tanzania umekataa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyomtangaza rais John Pombe Magufuli kama mshindi.

Viongozi wa upinzani wakiongozwa na Tundu Lissu wa chama cha CHADEMA na Freeman Mbowe wameitisha maandamano ya kitaifa kushinikiza kufanyika upya kwa uchaguzi mwingine kwa misingi kwamba uchaguzi wa Jumatano Oktoba 28 ulikumbwa na udanganyifu.

Maandamano hayo ya amani yasiyo na kikomo yameitishwa kuanzia Jumatano Novemba 2 hadi kuandaliwe marudio ya uchaguzi.

Tume ya uchaguzi nchini humo NEC ilimtangaza Magufuli wa chama tawala cha CCM kama rais mteule kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.

Tundu Lissu Aliibuka wa pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here