Madaktari katika hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta wamefaulu kurejesha mkono wa mtoto wa miaka saba aliyekatwa na mashine ya kukata nyasi mwanzoni mwa mwezi huu.
Mtoto huyo alikatwa kwa bahati mbaya akiwalisha ngombe nyumbani kwao kaunti ya Kiambu na kukimbizwa hospitalini humo huku mkono uliokatwa ukiwa umehifadhiwa kwenye sanduku la kutia baridi.
Madaktari walifaulu kuunganisha mkono huo baada ya saa nane za upasuaji na mtoto huyo sasa yuko salama na anaendelea kupata nafuu.
Upasuaji huo wa kuunganisha mkono na wa tano sasa kufanywa na madaktari hao katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta tangia mwezi wa pili mwaka 2018.