UKUMBI WA BOMAS KUPEWA MWONEKANO WA KIMATAIFA

0

Serikali imetangaza kuwa ukarabati wa kuufanya ukumbi wa Bomas of Kenya kuwa wa ngazi ya kimataifa utaanza ndani ya muda wa wiki mbili zijazo.

Baada ya ukarabati huo ukumbi huo utatambulika kwa jina la “Bomas international Convention Complex.”

Haya yamesemwa kupitia taarifa ya rais William Ruto kwenye mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika katika ikulu ya Nairobi siku ya Juma nne.

“Rais alitangaza kuwa ujenzi wa ukumbi wa Bomas utaanza ndani ya wiki mbili ikiashiria hatua muhimu katika mpango wa serikali wa kugeuza ukumbi huo kuwa kituo cha mikutano chenye hadhi ya kimataifa” sehemu ya taarifa hiyo ilieleza.

Tangazo hili linajiri siku moja baada ya serikali kupinga madai kuwa ukumbi huo umeuziwa raia wa Uturuki.

Ni madai yaliyoibuliwa na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua siku ya Jumapili kwa kudai kuwa serikali ilikuwa imeuza ukumbi huo kwa raia wa kigeni kutoka taifa la Uturuki.

Katibu katika idara ya utamaduni Ummi Bashir alifafanua kuwa ukumbi huo unasalia kumilikiwa na serikali ya Kenya.

Ukumbi wa Bomas unatambulika kwa kutumika kwa shughuli muhimu ikiwamo matangazo ya matokeo ya uchaguzi wa urais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here