UJUMBE WA GACHAGUA BAADA YA KUONDOLEWA AFISINI

0
GACHAGUA AKITOKA BUNGENI BAADA YA KUWASILISHA UTETEIZ WAKE DHIDI YA MSWAADA WA KUMTUMA NYUMBANI
GACHAGUA AKITOKA BUNGENI BAADA YA KUWASILISHA UTETEIZ WAKE DHIDI YA MSWAADA WA KUMTUMA NYUMBANI

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua amezungumza kwa mara ya kwanza kufuatia kutimuliwa kwake afisini na Bunge la kitaifa.

Naibu wa Rais ameweka ujumbe mtandaoni unaonukuu maandiko matakatafu saa chache baada ya kuondolewa afisini.

Kwenye ukurusa wake wa X Gachagua amenukuuu kitabu cha Wathesalonia 5: 8 kinachosema “Give thanks in all circumstances; for this is God’s will for you in Christ Jesus.”

Aidha amenukuu kitabu cha Jeremiah 30:19 “From them will come songs of thanksgiving and the sound of rejoicing. I will add to their numbers, and they will not be decreased; I will bring them honor, and they will not be disdained.” It is well.

Gachagua aliondolewa afisini hapo jana baada ya wabunge 281 kuunga mkono hoja dhidi yake ikilinganishwa na 44 waliopinga hoja hio.

“Sasa ninajukumu la kuwasilisha maazimio ya bunge hili kwa seneti. Naagiza karani kutayarisha stakabadhi hitajika kabla ya kuwasilishwa kwa seneti, alisema Spika Moses Wetangula baada ya kutangaza matokeo ya kura kuhusu hoja ya kutimua afisini Naibu wa Rais.

Seneti linachaguo la kubuni kamati spesheli kuchunguza madai dhidi ya Gachagua au kuchunguza madai hayo kama bunge nzima.

Iwapo kamati spesheli itabuniwa basi thuluthi mbili ya maseneta watatakiwa kupinga kura kuunga mkono ripoti ya kamati hio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here