Hatimye ripoti ya jopo la maridhiano BBI imepokezwa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga katika Ikulu ndogo ya rais kaunti ya Kisii.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Kenyatta amewataka wakenya kuisoma na kuelewa bila kuingiza siasa kabla ya kufanya uamuzi kupitia kwa kura ya maamuzi.
Kwa upande wake, Odinga amepuuzilia mbali madai kuwa ripoti hiyo inalenga kumpa tiketi ya kuingia Ikulu na pia kumpa nafasi Rais Uhuru Kenyatta kuwa waziri Mkuu baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Uzinduzi wa ripoti hiyo kwa umma utafanyika siku ya JUmatatu katika ukumbi wa BOMAS, Nairobi.