Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuenda kwenye likizo ya mwezi mmoja kuanzia Disemba 15 hadi Januari 16.
Katika arifa iliyotumwa kwa mabalozi wa Kenya katika mataifa mbalimbali na wizara ya mambo ya nje, rais hatakuwa afisini kwa majukumu rasmi kipindi hicho atakapokuwa kwenye likizo.
Wizara hiyo inasema majukumu kwa wizara mbalimbali yamekuwa mengi ikiwemo mikutano ya kimtandao kutokana na janga la corona.