Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kulegeza masharti ya kupambana na msambao wa virusi vya corona huku idadi ya virusi hivyo ikiendelea kupunguza.
Muda wa kafyuu umeongezwa kwa siku sitini zaidi ila mara hii itakuwa inaanza saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri kuanzia Kesho Jumanne.
Shule zitasalia kufungwa hadi usalama wa wanafunzi uhakikishwe kabla ya kuwaruhusu kurejelea masomo.
Thuluthi tatu ya waumini wataruhusiwa kuhudhuria ibada ila kwa kuzingatia masharti ya kuzuia msambao wa virusi hivyo huku idadi ya watu watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi na matanga imeongezwa kutoka 100 hadi 200.