UGANDA YATUMA JESHI SUDAN KUSINI

0

 

Uhasama unaoendelea kati ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na naibu wake wa kwanza Riek Machar umepelekea Uganda kutuma kikosi spesheli katika jiji kuu la taifa hilo.

Kwa mujibu wa mkuu wa jeshi nchini Uganda Muhoozi Kaneirugaba kikosi cha jeshi kitakuwa kinaimarisha usalama katika taifa hilo change Zaidi barani Afrika.

“Jeshi la Uganda limeingia Sudan Kusini ili kutoa ulinzi na tunatambua Rais Kiir pekee”, amesema Kaneirugaba kupitia mtandao wa X.

Kumekuwepo na vuta nkuvute nchini Sudan Kusini kufuatia serikali ya Rais Kiir kuwakamata na kuwazuilia mawaziri wawili na maafisa kadhaa wa jeshi kwa madai kuwa ni wandani wa Machar.

Kamata kamata hiyo imeonekana kuhujumu mkataba wa Amani wa mwaka 2018 uliotamatisha vita za kisiasa kati ya mirengo ya Kiir na Machar ambazo zilisababisha vifo vya watu laki nne.

Hii sio mara ya kwanza kwa Uganda kutuma jeshi nchini Sudan Kusini, kwani iliwahi kutuma jeshi mwaka wa 2013 na kisha kuwaondoa mwaka wa 2015 kabla ya kuwatuma tena mwaka wa 2016 baada ya vita kuzuka na kisha kondolewa.

Uganda imekuwa ange kusitisha vita nchini Sudan Kusini ikiwa na hofu ya wakimbizi kutorokea kwake iwapo vitachacha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here