Makachero wanaochunguza mauaji ya Kevin Omwenga katika eneo la Kilimani hii leo wanatazamiwa kupokea ripoti ya uchunguzi kuhusu bunduki tatu zinazomilikiwa na Chris Obure, mmoja wa washukiwa kwenye mauji hayo.
Obure pamoja na mshtakiwa mwenza katika mauji hayo Robert Ouko wamekuwa wakizuiliwa na Polisi tangu Jumatano iliyopita huku uchunguzi ukiendelea.
Polisi katika uchunguzi wao wanatafuta kufahamu ni vipi bunduki iliyotumika kumuua marehemu ilipatikana katika afisi za Obure usiku ambao Omwenga aliuawa.
Uchunguzi huo aidha unalenga kubaini iwapo bunduki zingine mbili zinazomilikiwa na Obure zina leseni.









