Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/008 wameandikisha taarifa katika makao makuu ya idara ya upelelezi DCI huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu mauaji hayo miaka kumi na mwili baadaye.
Mkurugenzi wa idara ya upelelezi nchini DCI George Kinoti anasema waathiriwa hao haswaa wale waliowapoteza wapendwao baada ya kuchomwa kwa kanisa la Kiambaa mjini Eldoret wamepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu wasiojulikana na hivyo kuchochea kuanzishwa kwa uchunguzi huo.
Kinoti amesema watafanya uchunguzi wa kina na kuwataja waliohusika na kupanga na kufadhili ghasia hizo kwa minajili ya kuwatendea haki walioathirika.
Idara hiyo imewahakikishia waathiriwa wao usalama wao wakati uchunguzi huo unaendelea.
Kesi hiyo zinafufuliwa siku chache baada ya wakili Paul Gicheru kujisalimisha katika mahakama ya kimataifa ya ICC baada ya waranti ya kukamatwa kutolewa dhidi yake.