Uamuzi kuhusu kufunguliwa kwa shule kutolewa juma lijalo

0

Uamuzi kuhusu kufunguliwa kwa shule unatazamiwa kutolewa wiki ijayo baada ya kikao cha wadau katika sekta ya elimu, amesema waziri wa elimu Profesa George Magoha.

Akizungumza baada ya mkutano na washikadau, Profesa Magoha anasema wamebuni kamati ndogo ya washikadau ambayo itabuni mwongozo wa ufunguzi wa shule.

Magoha amekiri kuwa changamaoto kuu inayowasubiri ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakaa umbali wa mita moja unusu wakiwa shuleni lakini akasema wanaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha hilo linaafikiwa.

Licha ya serikali kutagaza kuwa shule zitafunguliwa Jnauria, Magoha anasema huenda hilo likabadilika ikizingatiwa na msambao wa virusi vya corona nchini.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here