Tundu kumenyana na Pombe Tanzania

0

Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

Lissu amejinyakulia kura 405 akifuatiwa kwa mbali na mpinzani wake Lazaro Nyalandu aliyepata kura 36.

Muwaniaji mwingine aliyetaka kupeperusha bendera ya chama hicho Maryrose Majige alipata kura moja pekee katika uchaguzi uliofanyika jana usiku.

Jina la Lissu sasa litapelekwa kwenye kikao cha Mkutano Mkuu wa chama hicho utakaofanyika hii leo ili kupitishwa rasmi kumenyana na Rais John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi huo.

Tundu alirejea nchini Tanzania Jumatatu wiki iliyopita baada ya kukaa ughaibuni kwa zaidi ya miaka mitano aliponusurika jaribio la mauaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here