Tume ya mishahara SRC yapinga wabunge wa zamani kulipwa Sh100, 000

0

Tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma nchini SRC imepinga mipango ya kuwalipa wabunge wastaafu pensheni ya Sh100, 000 kila mwezi.

SRC kupitia taarifa imetaja hatua hiyo kama inayokiuka katiba na kuapa kumshawishi rais Uhuru Kenyatta kuukatalia mbali mswada huo uliopitishwa na bunge la kitaifa.

Aidha, tume hiyo imeelezea kuwa hatua hiyo itamuongezea mlipa ushuru mzigo zaidi na kwamba huenda watumishi wengine wa umma wakaitisha marupurupu kama hayo.

Kimsingi, tume hiyo inasema ndiyo iliyo na jukumu la kipekee kuamua mishahara na marupurupu ya watumishi umma na wala sio bunge.

Mswada huo unaosubiri saini ya rais unataka wabunge waliohudumu kati ya Julai, 1984 na Januari, 2001 kulipwa shilling laki moja kila mwezi kutokana juhudi zao la kulihudumia taifa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here