Trump aelekea mahakamani kupinga matokeo ya kura

0

Chama cha Republican nchini Marekani kimesema kinaelekea katika mahakama ya upeo nchini humo kuomba zoezi la kuhesabu kura linaloendelea kusitishwa.

Katika hotuba yake kutoka ikulu ya Rais, Rais Donald Trump amesema zoezi la kuhesabu kura limeingiliwa na kuna njama ya wizi wa kura baada yao kuibuka na ushindi katika jimbo la North Carolina.

Trump anayewania muhula wa pili kupitia kwa chama hicho cha Republican ameelezea imani yake kuwa yeye ndiye ameibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo uliofanyika hapo jana licha ya kuwa zoezi la kuheabau kura bado linaendelea.

Kupitia kwa ukurasa wa Twitter awali, Trump aliweka bayana kuwa mpinzani wake wa chama cha Democrratic Joe Biden alikuwa anapanga kuiba kura na kuapa kutokubali njama hiyo kufaulu..

Hata hivyo katika kikao na wanahabari mapema awali, Biden ameelezea matumaini yake kuwa ataibuka mshindi.

Hadi sasa Biden anaongoza kwa kura 224 dhidi ya 213 za Trump za Baraza Maalum la Kumchagua Rais (Electoral college) na mshindi anahitaji kupata kura 270 miongoni mwa wajumbe 538.

Kura zitakamilika kuhesabiwa hii leo saa moja jioni, saa za Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here