Transparency International yapinga pensheni kwa wabunge wastaafu

0

Shirika la Transparency International limejiunga na wanaopinga mswada unaolenga kuwalipa wabunge wa zamani pensheni ya Sh100, 000 kila mwezi.

 TI katika taarifa imesema taifa hili litatumia kiasi kikubwa cha pesa kugharamikia malipo hayo kwa wabunge wastaafu kwani kila mwaka wabunge hao watakuwa wanalipwa Sh180M.

Shirika hilo vile vile limekosoa bunge kwa kupitisha mswada huo likisema tume ya mishahara SRC ndiyo ina jukumu la kikatiba kuamua mishahara wanayopaswa kulipwa watumishi wa umma.

Haya yanajiri siku moja baada ya SRC kupinga hatua hiyo na kuapa kumshauri rais Uhuru Kenyatta kuukatalia mbali mswada huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here