SUDAN YAPIGA MARUFUKU UAGIZAJI WA BIDHAA ZA KENYA

0
RAIS RUTO ALIPOKUTANA NA MKUU WA RSF Mohamed Hamdan Daglo
RAIS RUTO ALIPOKUTANA NA MKUU WA RSF Mohamed Hamdan Daglo

Mzozo wa Kidiplomasia kati ya Kenya na Sudan imechukua mkondo mwingine Serikali ya Sudan sasa ikipiga marufuku uagizaji wa bidhaa zote zinazotengenezwa humu nchini.

Katika agizo rasmi, Wizara ya Biashara na Ugavi ilielekeza pande zote zinazohusiana na uagizaji wa bidhaa kutekeleza agizo hilo mara moja.

“Uagizaji wa bidhaa zote zinazotoka katika nchi ya Kenya kupitia bandari zote, vivuko, viwanja vya ndege na maduka umesitishwa, kuanzia tarehe hii hadi ilani nyingine itakapotolewa,” Kaimu Waziri Omar Ahmed Mohamed Ali amesema.

“Pande zote zinazohusika lazima zitekeleze uamuzi huo.” Ameongeza Ali.

Uamuzi huo umefuatia azimio la Baraza la Mawaziri la Sudan lililopitishwa kutokana na ushirikiano wa Kenya na Kundi la Waasi wa RSF ambayo serikali ya Sudan inadai imetekeleza mauaji na uhalifu nyingine nchini humo.

Baraza Kuu la Sudan pia linashutumu Nairobi kwa kufadhili shughuli za RSF na washirika wao.

RSF na washirika wao walitia saini mkataba wa kuanzisha serikali ya umoja katika taifa hilo lililokumbwa na vita la Afrika Kaskazini.

Kutiwa saini kwa mkataba huo katika ukumbi wa Mikutano ya KICC kulikuwa hitimisho la mazungumzo ya siku nne yaliyoandaliwa humu nchini.

Sudan ilisema katika taarifa kwamba Kenya pia ilikiuka kanuni za ujirani mwema kwa kuruhusu RSF na washirika wao kuendeleza shughuli zao humu nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here