Spika wa Migori na wenzake wakamtwa kwa ufisadi

0

Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC wamemshika spika wa bunge la kaunti ya Migori, naibu wake pamoja na maafisa wengine kuhusiana na madai ufisadi.

Spika wa bunge hilo Boaz Okoth, naibu wake Mathews Chacha wamekamatwa pamoja na wanakandarasi wengine kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa pesa za kaunti.

Washukiwa hao wanadaiwa kushirikiana kutekeleza uhalifu wa kiuchumi na kukosa kuzingatia kanuni za ununuzi.

Wengine ni karani wa bunge hilo Tom Opere, naibu Emanuel Aballa na meneja wa mauzo Steve Okello.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here