Spika wa bunge la Migori aachiliwa kwa dhamana

0

Spika wa kaunti ya Migori Boaz Okoth na washukiwa wengine kumi na wanne wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi million tatu au shilingi laki tatu pesa taslimu baada ya kukanusha mashtaka dhidi yao.

Akitoa agizo hilo, hakimu mkuu wa Mahakama ya Kisumu Peter Gesore amewaagiza kutohitilafiana na ushaidi na kuwataka kurejea mahakamani tarehe 15 Februari mwakani kwa vikao vya kutajwa kwa kesi hiyo kabla ya kuanza kusikilizwa tarehe 22 Machi hapo mwakani.

Okoth, naibu wake Mathews Chacha, karani wa bunge la kaunti hiyo Tom Opere na washukiwa wengine wanatuhumiwa kushirikiana kuiba shilingi milioni 44 pesa za umma kati ya mwezi Mei na Oktoba mwaka 2019.

Washukiwa ambao walikesha korokoroni usiku kucha baada ya kukamatwa jana wamekabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo kushirikiana kutekeleza uhaliu wa kiuchumi, matumizi mabaya ya mamlaka na ufisadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here